Kanga
Katika visiwa vya Zanzibar, kanga ni miongoni mwa vazi maarufu ambalo watu hulitumia katika shughuli zao mbali mbali kama; kusalia, kupikia, kulalia, kuvishiwa bibi harusi na hata kuendea msibani. Kuna aina mbali mbali za kanga lakini ni vyema tukaijua kanga ya KISUTU.
Kisutu cha asili ni chenye rangi ya kahawia kwa weusi lakini siku hizi kumejitokeza kisutu cha rangi mbali mbali ambacho hujulikana kama ni aina mpya ya kanga hiyo. Miongoni mwa rangi hizo ni pamoja na kisutu kahawia kwa weusi, kijani kwa weupe, cheupe kwa wekundu na hata buluu bahari kwa weupe.
AINA ZA KANGA YA KISUTU
Hiki ni kisutu cha rangi kahawi kwa weusi. Kisutu cha aina hii ndicho cha asili kinachojulikana kwa muda mrefu ambacho hutumika kuwakilisha utamaduni wa Wazanzibari na hasa katika sherehe za harusi.
(Kabati la kanga.wordpress.com)
Maharusi wa zamani walivaa kisutu kwa namna yao ila siku hizi hushonwa na kutengenezwa maalumu na kuwa nguo kamili ya bibi harusi.
(MWANAMKE PENDEZA NA MISHONO- youtube).
Vile vile kisutu hutumika kama pambo katika kitanda cha maharusi wa Kizanzibari.
Angalia video inayohusu asili na historia ya vazi la kanga.
https://youtu.be/CYUyToOop4E
No comments:
Post a Comment